Watu 274 wauawa katika mashambulio ya jeshi la Israel kwenye kambi za wakimbizi katikati mwa Ukanda wa Gaza
2024-06-10 08:55:57| cri

Idara ya afya ya Ukanda wa Gaza ya Palestina imesema watu 274 wameuawa na wengine 698 kujeruhiwa kufuatia mashambulio ya jeshi la Israel dhidi ya kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza jumamosi iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na Idara hiyo imesema, waathirika wengi walikuwa bado wamenasa chini ya vifusi au wamelala barabarani, na waokoaji hawakuweza kuwafikia.

Habari zinasema, siku hiyo hiyo, jeshi la Israel liliwaokoa Waisraeli wanne waliokuwa wamezuiliwa hapo awali na Kundi la Hamas katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat.