Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka jamii ya kimataifa kuokoa bahari
2024-06-10 08:58:23| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kuokoa bahari.

Guterres amesema hayo katika ujumbe wake wa Siku ya Bahari Duniani iliyoadhimishwa Juni 8. Amesema bahari zinaendeleza na kuboresha maisha ya viumbe vyote duniani, lakini kwa sasa zinakabiliwa na hali mbaya, na wa kulaumiwa ni binadamu.

Amesema athari za mabadiliko ya tabianchi zinasababisha kuongezeka kwa kina cha maji, ambacho sio tu ni tishio kwa visiwa vidogo na maeneo ya pwani, bali pia kinasababisha matukio makubwa ya hali ya hewa yanayoathiri jamii nzima.

Akisisitiza fursa muhimu za mkutano wa mwaka huu wa Hatma ya Bahari wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika nchini Ufaransa, Guterres ametoa wito kwa serikali, wafanyabishara, wawekezaji, wanasayansi na jamii ya kimataifa kuchukua hatua zinazoweza kurejesha na kulinda viumbe vya baharini na mfumo wa ikolojia wa pwani.