Msako waendelea kutafuta ndege iliyopotea ikiwa na makamu wa rais wa Malawi
2024-06-11 08:38:33| cri



Msako unaendelea nchini Malawi kutafuta ndege iliyotoweka ikiwa na makamu wa rais wa nchi hiyo Bw. Saulos Chilima na watu wengine tisa.

Ndege hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Malawi ilipotea kwenye rada Jumatatu asubuhi na haikutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mzuzu kaskazini mwa nchi hiyo, ambako makamu wa rais alitakiwa kwenda kushiriki kwenye mazishi ya Waziri wa Sheria wa zamani Ralph Kasambara. 

Jeshi la Ulinzi la Malawi na Jeshi la Polisi la Malawi, pamoja na vyombo vingine vya usalama, vinaendelea na msako katika msitu wa Chikangawa kwenye kitongoji cha Mzuzu, sehemu ambayo ndege hiyo inashukiwa kupotea.