Tanzania iko tayari kuingia katika soko la graphite baada ya mradi wa Bunyu kuanza kazi
2024-06-11 10:53:16| cri

Sekta ya madini nchini Tanzania ambayo inaendelea kufanyiwa mageuzi, sasa ina miradi miwili mikubwa ya madini ya graphite ambayo iko tayari kwa uzalishaji. Mradi wa Bunyu mkoani Lindi uliosubiriwa kwa muda mrefu hatimaye umeanza uzalishaji, wakati kampuni moja ya Australia, ilipotangaza kusafirisha kwa mafanikio shehena ya kwanza ya graphite kutoka mgodi huo. Usafirishaji huo unaashiria hatua muhimu kwa mradi huo tangu ulipoanza kufanya kazi.

Habari za kuingia sokoni kwa mgodi huo, zimekuja wakati bei ya madini hayo katika soko la dunia likiendelea kuwa kubwa.