Nchi za Afrika zataka kuharakisha mageuzi ya Baraza la Usalama la UM
2024-06-11 08:37:41| CRI

Kamishna wa Masuala ya Siasa, Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika Bankole Adeoye amesisitiza haja ya mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, huku akitoa wito wa mazungumzo kati ya nchi za Afrika kuharakisha hatua ya mageuzi.

Adeoye amesema hayo katika Mkutano wa 11 wa Mawaziri wa Kamati ya Umoja wa Afrika wa Wakuu wa Nchi Kumi na Serikali kuhusu mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika katika mji mkuu wa Algeria, Algiers. Pia alitaja majukumu makuu mengine barani Afrika, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kunyamazisha silaha, kupambana na ugaidi, kufikia maingiliano ya bara na kuhakikisha uwakilishi bora katika ngazi ya kimataifa.

Timothy Musa Kabba, Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa wa Sierra Leone, ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa kamati hiyo, amesisitiza umuhimu wa kufikia makubaliano ya Afrika juu ya mageuzi ya Baraza la Usalama, akiwataka viongozi wa Afrika kuharakisha mazungumzo yanayolenga kufikia lengo hili.