Idadi ya wakimbizi nchini Sudan yapita milioni kumi wakati mapigano nchini humo yakiendelea
2024-06-11 22:51:55| cri

Shirika la kimataifa la uhamiaji limesema mapigano nchini Sudan yamesababisha robo ya idadi ya watu nchini humo kukimbia makazi yao, na sasa idadi ya wakimbizi nchini Sudan imezidi milioni kumi.

Licha ya hayo, Wasudan wengine zaidi ya milioni mbili wamekimbilia nchi za nje kama vile Chad, Sudan Kusini na Misri.