Uganda kuwa ya pili kwa uchumi unaokua kwa kasi kwenye eneo la Afrika Mashariki kwa mwaka huu
2024-06-12 22:34:52| cri

Benki ya Dunia imesema Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) zitakuwa na uchumi wa pili unaokua kwa kasi katika eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zikiwa na kasi ya ukuaji wa asilimia 6.0 kwa mwaka 2024.

Matarajio yaliyotolewa jana Juni 11 na benki ya dunia mjini Washington, yanaonesha kuwa mwaka huu Rwanda itakuwa nchi yenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi katika Afrika Mashariki (asilimia 7.6), Tanzania kasi ya ukuaji itakuwa asilimia 5.4, ikizifuata Uganda na DR Congo huku Kenya ikitarajiwa kukua kwa asilimia 5.0. Uchumi wa Burundi unatarajiwa kukua kwa asilimia 3.8, Somalia ikiwa na asilimia 3.7 na Sudan Kusini kwa asilimia 2.0.

Maendeleo chanya ya kiuchumi katika kanda hiyo pia yametajwa kuwa yatasababisha kuongezeka kwa biashara na uboreshaji wa mapato ya watu kutokana na soko la bidhaa kufufuka baada ya janga la Covid-19.