Watu 86 wakiwemo watoto 21 wamefariki baada ya boti kuzama katika Mto Kwa, moja ya matawi ya Mto Kongo, katika mkoa wa Mai-Ndombe, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ajali hiyo ilitokea majira ya saa tano usiku kwa saa za huko karibu na kijiji cha Lediba, kwamba boti hiyo ilikuwa inatoka mji wa Mushie kuelekea mji mkuu wa DRC, Kinshasa.
Vyanzo vya habari pia vimesema watu 185 wameokolewa, na kuonya kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka.