Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) jana limesema, wahamiaji zaidi ya 49 wamefariki na wengine 140 hawajulikani walipo baada ya meli waliyopanda kupinduka katika pwani ya Yemen.
Shirika hilo limesema miongoni mwa watu waliofariki ni wanawake 31 na watoto sita waliokimbia vita, ukame, na matatizo ya kiuchumi katika nchi zao.
Msemaji wa IOM Mohammedali Abunajela amesema, Janga hilo ni ukumbusho mwingine wa haja ya dharura ya kufanya juhudi kwa pamoja ili kushughulikia changamoto za uhamiaji zisizo za kawaida.