China yapenda kufanya juhudi endelevu kukuza mabadilishano ya utamaduni na maendeleo ya amani ya dunia
2024-06-12 08:45:18| cri

Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika ijumaa iliyopita kilipitisha kwa kauli moja azimio lililopendekezwa na China la kuanzisha "Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Utamaduni" itakayoadhimishwa Juni 10 kila mwaka.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema, China inapenda kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa kutekeleza kikamilifu azimio hilo na kufanya juhudi endelevu kukuza maelewano na kujifunza kwa pamoja kati ya utamaduni na kuhimiza maendeleo ya amani duniani.

Bw. Lin pia amesema, hivi sasa, wakati mustakabali na hatma ya nchi zote zina uhusiano wa karibu, uvumilivu, kuishi pamoja, kubadilishana na kujifunza kati ya utamaduni mbalimbali kunachukua nafasi isiyoweza kupuuzwa katika kukuza mchakato wa kisasa wa jamii ya binadamu na kustawisha bustani ya utamaduni wa dunia.