Rais wa China ajibu barua ya profesa wa Chuo Kikuu cha Tsinghua
2024-06-12 16:02:55| cri

Rais Xi Jinping wa China ametia moyo Andrew Chi-Chih Yao, profesa wa Chuo Kikuu cha Tsinghua, kuzidi kutoa mchango katika maendeleo ya kuandaa watu wenye vipaji wa China na uvumbuzi wa kisayansi.

Rais Xi amesema hayo katika barua ya jibu iliyotumwa hivi karibuni kwa Yao wa Akademia ya Sayansi ya China aliyerudi nchini China na kuanza kazi yake ya ualimu katika chuo kikuu cha Tsinghua miaka 20 iliyopita.

Katika barua yake, Rais Xi alitoa salamu kwa Yao akipongeza mafanikio aliyopata katika sekta ya ualimu na uvumbuzi wa kisayansi katika miaka 20 iliyopita ambapo alibadilisha upendo wake kwa taifa kuwa ahadi ya kuihudumia nchi.

Profesa Yao aliyefundisha katika vyuo vikuu vya Marekani kwa muda mrefu, alirudi China mwaka 2004 na kujiunga na Chuo Kikuu cha Tsinghua.