Biashara ya nje ya China yaendelea kupiga hatua ikipanua soko kwa bidhaa mpya
2024-06-13 10:46:23| cri

Kwa mujibu wa kampuni ya utengenezaji wa magari ya China BYD, katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka huu, mauzo ya nje ya magari ya nishati mpya ya BYD yaliyofikia laki 17.6, yakitimiza ukuaji bora katika mauzo ya nje ya magari. Kabla ya hapo, Shirikisho la Ujumbe wa Soko la Magari la China lilitoa takwimu zikionesha kuwa toka mwezi wa Januari hadi Mei mwaka huu, mauzo ya nje ya magari ya China yalifikia milioni 2.45 yakiongezeka kwa asilimia 27 ikilinganishwa na mwaka jana. Mauzo ya nje ya magari ya nishati mpya yamekuwa nguvu kuu inayohimiza ongezeko la biashara ya nje ya China.

Hivi sasa, hali ya siasa za kijiografia duniani inazidi kuwa ya wasiwasi, ukuaji wa uchumi unaendelea kuwa duni, huku biashara ya dunia ikidumisha mwelekeo wa kufufuka kwa kasi mdogo tangu mwaka jana. Wakati huohuo, baadhi ya nchi za magharibi zinapiga kelele kuhusu hoja zinazojulikana kama “Kutenganisha” na “Kuondoa Hatari” na kuleta vikwazo vya biashara duniani. Biashara ya nje ya China ikikabiliwa na hali ngumu ya nje, inaendelea kukua kwa kasi hasa katika bidhaa za aina tatu mpya ambazo ni magari ya umeme, betri ya lithiamu na betri ya jua, huku ikipata wateja wengi zaidi duniani kote na kuonesha nguvu ya ushindani ya “Utengenezaji kwa Teknolojia ya China”.

Takwimu zilizotolewa na serikali ya China zinaonesha kuwa katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka huu, thamani ya jumla ya mauzo na maagizo ya bidhaa kutoka nje ya China ilifikia Yuan Trilioni 17.5 yakiongezeka kwa asilimia 6.3 ikilinganishwa na mwaka jana. Inastahili kufuatiliwa ni kwamba kasi ya ongezeko la mauzo na maagizo ya bidhaa kutoka nje mwezi Mei ilifikia asilimia 8.6 ikiongezeka kwa asilimia 0.6 ikilinganishwa na mwezi wa Aprili. Kutoka mabadiliko ya kigezo hicho katika robo ya kwanza ya mwaka huu hadi kigezo kilichoongezeka mwezi Aprili na Mei, biashara ya nje ya China imepiga hatua ya kurejesha ukuaji.