Ofisa wa kundi la Hamas asema kundi hilo halijatoa marekebisho mapya kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano
2024-06-13 10:41:44| cri

Ofisa wa kundi la Hamas amesema kuwa kundi hilo halijatoa marekebisho mapya kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza lililotolewa na Marekani, ila limesisitiza ahadi zilizotolewa na pande husika katika mazungumzo ya kusitisha vita yaliyofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Pia amesema Israel inaweza kuanzisha vita tena kama mazungumzo yatashindwa katika siku zijazo na kundi la Hamas linataka jumuiya ya kimataifa ihakikishe Israel haifanyi hivyo na kutekeleza hatua mbalimbali katika kipindi tofauti kufuata upangaji wa pendekezo la kusitisha vita. Linachotafuta kundi hilo ni vita kusitishwa daima katika Ukanda huo, jeshi la Israel kuondoka kutoka eneo hilo, watu wa Gaza waliokimbia kurudi kwenye makazi yao, Ukanda huo kujengwa upya na vikwazo dhidi yake kuondolewa.