Watu 80 wafariki katika ajali ya kuzama kwa meli nchini DRC
2024-06-13 10:40:11| cri

Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetoa taarifa kwenye mtandao wa kijamii ikisema ajali ya kuzama kwa meli ilitokea usiku wa tarehe 10 mwezi huu katika Jimbo la Mai-Ndombe, magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha vifo visivyopungua 80. Rais Felix Tshisekedi wa DRC ameomboleza vifo vya wahanga hao na kuagiza idara husika kufanya kazi ya uokoaji na uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo.