Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamepelekwa kulinda raia dhidi ya mapigano kati ya makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo.
Naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema jana kuwa, wafuasi wa makundi ya Zaire na CODECO wamepigana katika eneo la machimbo ya madini lililoko kilomita 40 kutoka mji wa Bunia, mkoa wa Ituri, hivyo walinzi wa amani wa Umoja huo wamepelekwa ili kuwalinda raia.
Amesema tangu tarehe 25 Mei, kundi la ADF lilifanya mashambulio mfululizo katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100.