Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya moto Kuwait yafikia 49
2024-06-13 08:45:56| CRI

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kuwait imesema, idadi ya watu waliofariki katika ajali ya moto iliyotokea jumatano asubuhi katika jengo la makazi lililoko eneo la Mangaf, kusini mwa Mji wa Kuwait, imefikia 49.

Kadhi wa Kuwait Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ameagiza uchunguzi ufanyike mara moja kujua chanzo cha moto huo, na kuahidi kuwawajibisha wote watakaohusika na ajali hiyo.

Naibu wa kwanza wa Waziri Mkuu wa Kuwait Sheikh Fahad Yusuf Al-Sabah, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya Ndani, wameagiza kushikiliwa kwa watu wanaohusika na ajali hiyo, akiwemo mmiliki wa jengo hilo, mpaka timu ya uchunguzi ya mahakama itakapomaliza uchunguzi wake.

Pia ameziagiza idara husika za serikali kukagua na kushughulikia ukiukaji wa kanuni za ujenzi ili kuepuka kutokea kwa ajali kama hiyo.