China yatoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Makamu wa Rais wa Malawi
2024-06-13 08:42:46| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema jana kwamba, China imetoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Makamu wa Rais wa Malawi Bw. Saulos Chilima na wahanga wengine kutokana na ajali ya ndege iliyotokea jumatatu wiki hii.

Bw. Lin amesema, katika wakati huu mgumu, serikali na watu wa China wanasimama kidete na serikali na watu wa Malawi, na anaamini kuwa, chini ya uongozi wa rais Lazarus Chakwera, Malawi itaweza kuondokana na matatizo na kuondoka kwenye huzuni.

Katika hotuba yake aliyoitoa jumanne, Rais Chakwera alisema ndege ya jeshi la nchi hiyo iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais na watu wengine 9 ilianguka jumatatu, na mabaki ya ndege hiyo yamepatikana, huku watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo wamefariki.