Ubunifu unaoongozwa na vijana umetajwa kuwa unaweza kuhimiza maendeleo ya kilimo nchini Rwanda na kupunguza hasara inayowakumba wakulima baada ya kuvuna.
Kampuni ya Freza NanoTech yenye makao yake nchini Uganda, imekuja na suluhisho la kibunifu linalojumuisha uundaji wa mifuko yenye vimeng’enya vinavyozuia kuharibika kwa matunda, kuwezesha matunda na mboga kukaa safi kwa hadi siku 31 bila kuwekwa kwenye jokofu. Samantha Ainembabazi, mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Freza Nanotech amesema wataunganisha teknolojia na kilimo, na kujitahidi zaidi katika kuhifadhi matunda na mboga, teknolojia inayofanya kazi kwa kupunguza kasi ya kukomaa.