Serikali ya Tanzania kujipanga na kuja na sheria ya kupambana na ukatili wa kijinsia
2024-06-13 10:43:30| cri

Naibu waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Jumanne Sagini amesema Serikali ya Tanzania inafanya tathmini kwa kushirikiana na wizara nyingine na Asasi za Kiraia kubaini kama kuna haja ya kuwa na sheria mahususi ya ukatili wa kijinsia au kuboresha sheria zilizopo.

Alisema tathmini hiyo ikikamilika, itasaidia serikali kufanya uamuzi sahihi kuhusu suala la kutunga sheria mahsusi kwa makosa ya ukatili wa kijinsia. Amesema Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sheria ya Ndoa, Sheria ya Mtoto, Sheria ya Makosa ya Mtandao na Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu zina vifungu vinavyozuia makosa ya ukatili wa kijinsia na vifungu vinavyohusika na makosa ya ukatili wa kijinsia.

Kutokana na kuendelea kushamiri kwa vitendo vya ukatili lina ya kuwepo kwa sheria hizo, serikali imeamua kukaa na wadau kutafakari.