Tanzania kuzindua huduma za treni ya SGR kati ya Dar es salaam na Morogoro
2024-06-13 22:42:18| cri

Huduma za treni za reli ya Standard gauge (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro zimeanza rasmi nchini Tanzania, hatua ambayo inaashiria maendeleo makubwa katika miundombinu ya usafiri nchini Tanzania.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli Tanznaia TRC Bw. Masanja Kadogosa amesema hatua hiyo itaimarisha uunganishaji na ufanisi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Bw. Kadogosa aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji yenye kauli mbiu “Twende Tukapande Treni Yetu, Tuitunze, Tuithamini”. Amesema wamezindua kampeni hiyo ili kuhamasisha watu wengi zaidi kusafiri kwa treni hiyo ili wakati huduma zinapoanza kati ya Dar es alaam na Dodoma, watu wengi wawe na ufahamu kuhusu treni hiyo.