Hafla ya makabidhiano ya Hospitali ya Lesotho iliyojengwa kwa msaada wa China yafanyika mjini Maseru
2024-06-14 08:41:04| CRI

Hafla ya kukabidhi mradi wa Hospitali ya Lesotho na kliniki ya macho ya Maseru uliotekelezwa kwa msaada wa China imefanyika Alhamisi mjini Maseru.

Katika hafla hiyo, Waziri Mkuu wa Lesotho Bw. Matt Kane amesema baada ya kukamilika na kuanza kufanya kazi, hospitali hiyo itatoa huduma thabiti za matibabu kwa wakazi wa sehemu hiyo na maeneo ya jirani.

Waziri wa Afya wa nchi hiyo Bw. Selibe Mochoboroane amesema Lesotho inatarajia kuchukua hospitali ya Maseru kuwa mfano mzuri wa kuigwa, na kuhimiza kiwango cha matibabu na hospitali kote nchini humo kupanda katika ngazi mpya.

Kaimu Balozi wa China nchini Lesotho Lv Liangzhong amesema, China itaendelea kufuata wazo la ujenzi wa Jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja, kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Lesotho katika sekta mbalimbali, ili kunufaisha nchi na watu wa pande hizo mbili.