Shirika la Umeme la Zambia limeichagua kampuni ya PowerChina International ya China kujenga mradi wa umeme wa jua wa kilowati 800 katika wilaya ya Chisamba katikati ya nchi hiyo.
Mradi huo unaowezeshwa na Shirika la Nishati la Kariba Kaskazini, unalenga kuboresha uwezo wa upatikanaji wa umeme nchini Zambia na kufungua fursa za kiuchumi kwa eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika hilo kwenye ukurasa wake wa Facebook, tayari kampuni hiyo ya China imeanza ujenzi katika eneo husika baada ya kukamilika kwa mafanikio kwa tathmini ya kimazingira iliyofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Zambia, na kwamba michoro yote katika mradi huo umekamilika na inasubiri kupitishwa kwa waraka wa mwisho kutoka kwa wagavi.
Hivi karibuni, Waziri wa Nishati wa Zambia Peter Kapala alisema serikali ya nchi hiyo inatekeleza hatua za muda mfupi na muda mrefu ili kukabiliana na athari ya uhaba wa umeme nchini humo.