Watu 30 wauawa na waasi wa ADF mashariki mwa DRC
2024-06-14 08:39:50| cri

Msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika eneo la Beni Bw. Mak Hazukay amethibitisha kuwa, watu 30 wameuawa mwishoni Jumatano usiku katika shambulizi lililofanywa na waasi wa kundi la ADF, ambao hivi karibuni walianzisha mfululizo wa mauaji mashariki mwa nchi hiyo.

Amesema waasi hao walifanya mashambulizi katika kijiji cha Mayikengo, eneo la Lubero, mkoa wa Kivu Kaskazini, na kwamba wengi wa watu waliouawa ni wanawake na watoto waliouawa kwa kukatwa na mapanga.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu imesema, shambulio hilo limekuja siku chache baada ya mashambulio mabaya ya kundi hilo katika eneo la jirani la Beni, ambapo watu karibu 57 waliuawa kati ya tarehe 3 hadi 8 mwezi huu.