China yapenda kushirikiana na dunia kunufaika na maendeleo ya ubora wa juu
2024-06-14 09:08:34| cri



Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lin Jian jana amezungumzia hatua ya Benki ya Dunia kuinua makadirio ya ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka 2024, na kusisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na dunia kunufaika na maendeleo ya ubora wa juu, na kuhimiza zaidi maendeleo ya utandawazi wa kisiasa duniani.

Ripoti ya Makadirio ya Uchumi wa Dunia iliyotolewa hivi karibuni na Benki ya Dunia iliinua makadirio ya ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka 2024 hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.5.