Pato la taifa la Tanzania liliongezeka kwa zaidi ya Sh7.1 trilioni mwaka 2023
2024-06-14 10:31:53| cri

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji) wa Tanzania Prof. Kitila Mkumbo, amesema pato la ndani la Tanzania (GDP) lilikua kwa Sh7.1 trilioni mwaka wa 2023, na kufikia Sh148.3 trilioni mwaka 2023.

Akiwasilisha bungeni maelezo kuhusu hali ya uchumi wa taifa, Prof. Mkumbo amesema kiasi hicho kinawakilisha ukuaji wa asilimia 5.1 ikilinganishwa na Sh141.2 trilioni za mwaka 2022. Hata hivyo amesema faida za ukuaji hazijagawanywa kwa usawa, hasa miongoni mwa wananchi maskini.

Prof. Mkumbo alisema uchumi wa nchi unaendelea kuwa thabiti licha ya misukosuko ya kimataifa ambayo ni pamoja na matokeo ya janga la Covid-19 kwenye minyororo muhimu ya usambazaji, mabadiliko ya tabia nchi, na mivutano ya kisiasa na migogoro duniani.

Pia amesema kumekuwa na ongezeko la thamani ya mauzo ya nje kwa mwaka kutoka dola milioni 975 za mwaka 2000, hadi dola za kimarekani bilioni 5.63 za mwaka 2020, na kufikia dola za kimarekani bilioni 8.2 za mwaka 2023.

.