Chama cha ANC cha Afrika Kusini chatazamia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa
2024-06-14 10:30:51| cri

Katibu Mkuu wa chama tawala cha Afrika Kusini African National Congress (ANC) Bw. Fikile Mbalula amesema chama chake kinatarajia kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Bw. Mbalula aliyasema hayo siku moja kabla ya kikao cha kwanza cha bunge la taifa, kinachotarajiwa kufanyika leo Ijumaa ya kumchagua rais wa Afrika Kusini kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Amesema ANC inatazamia kuanza kwa bunge la saba la kidemokrasia na kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, na tarehe ya kuapishwa kwa rais wa Afrika Kusini imepangwa Juni 19. Bunge la Afrika Kusini pia limetangaza kuwa rais mteule wa nchi hiyo ataapishwa mjini Pretoria Jumatano wiki ijayo.