Ujumbe wa AU nchini Somalia wasema kupunguzwa kwa wanajeshi hakutaacha "ombwe la usalama" nchini Somalia
2024-06-17 08:38:47| CRI

Mjumbe mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Somalia Bw. Mohamed El-Amine Souef, amewahakikishia watu wa Somalia kuwa kuondolewa kwa wanajeshi wa Umoja wa Afrika nchini humo hakutasababisha "ombwe la usalama".

Bw. Souef amesema Umoja wa Afrika hautaitelekeza Somalia hata kama Ujumbe wa Mpito wa AU nchini Somalia (ATMIS) unajiandaa kuondoa wanajeshi 4,000 zaidi ifikapo mwisho wa mwezi Juni.

Amesema mpito huo utaratibiwa vyema kati ya nchi wanachama wa shirikisho la Somalia (FMS), serikali ya Somalia, na washirika wa kimataifa.

Kwa mujibu wa azimio namba 2710 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ATMIS inatakiwa kuondoa askari 4,000 katika awamu ya tatu na nafasi yake kuchukuliwa na jeshi la Somalia.