Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Iran, rais wa mpito wa Iran Bw. Mohammad Mokhber amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Abdul Latif Rashid wa Iraq, ambapo pande mbili zimeahidi kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.
Bw. Mokhber amesema kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi kutaboresha uhusiano wa kisiasa, huku akibainisha kuwa pande mbili zinaweza kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kwa kuondoa vizuizi kwenye ushirikiano kati ya sekta binafsi za nchi hizo mbili.
Bw. Mokhber pia ameipongeza Iraq kwa hatua zake zenye ufanisi, busara na heshima katika jukwaa la kikanda na kimataifa ikiwemo hatua kuhusu suala la Gaza.
Rais wa Iraq amesisitiza kuwa serikali yake inafanya juhudi kuboresha kiwango cha ushirikiano na Iran katika nyanja zote.