Rais wa Namibia atoa wito wa kujitolea kwa elimu bora barani Afrika
2024-06-17 08:38:10| CRI

Rais Nangolo Mbumba wa Namibia ametoa wito wa kuhakikisha elimu bora inapatikana barani Afrika, na kusema bara la Afrika litanufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwekeza katika elimu na vijana, kama ilivyoainishwa kwenye Ajenda ya Afrika kuelekea mwaka 2063.

Rais Mbumba aliungana na wanamibia na bara zima la Afrika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika, akisisitiza umuhimu wa siku hiyo kwa kukumbuka ujasiri wa vijana wa Afrika Kusini ambao walipinga mfumo wa kibaguzi wa elimu.

Akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu ya "Elimu kwa watoto wote barani Afrika: wakati ni sasa", Rais Mbumba amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora.