Watu wanne wafariki na wengine wanne wajeruhiwa katika ajali ya barabarani kaskazini mwa Tanzania
2024-06-17 09:20:34| CRI

Takriban watu wanne wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali ya kugongana kwa basi na lori iliyotokea jumamosi usiku katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga kaskazini mwa Tanzania.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Bw. Maketi Msangi amesema ajali hiyo ilitokea saa tatu usiku wa Jumamosi katika kijiji cha Tanganyika kando ya barabara kuu ya Dar es Salaam-Arusha wakati basi hilo dogo likifanyiwa matengenezo baada ya kupata hitilafu za kiufundi. Dereva wa lori hilo alitoroka baada ya ajali hiyo, na polisi wanamsaka.