Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya mataifa 8
2024-06-18 14:10:10| cri

Tanzania imejipanga kuandaa mashindano mapya ya soka ya wanawake ya timu nane Juni mwaka huu.

Mashindano hayo yanaandaliwa na Shirika la Homeless World Cup na yatafanyika Arusha kwa siku mbili Juni 29 na 30. Kando na Tanzania mwenyeji, timu zilizothibitishwa kushiriki ni pamoja na Kenya, Malawi, Afrika Kusini, Namibia, Uganda, Zambia na Zimbabwe.