Waziri Mkuu wa China asisitiza kudumisha kasi chanya iliyopatikana katika maendeleo ya utulivu ya uhusiano kati ya China na Australia
2024-06-18 14:08:55| cri

Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana jumatatu amesisitiza umuhimu wa kudumisha na kuendeleza kasi nzuri ya sasa ya uhusiano wa pande mbili kati ya China na Australia.

Akizungumza na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wakuu wa China na Australia, Li Qiang amesema alama muhimu ya uhusiano wa pande hizo mbili ni ushirikiano wa kunufaishana, na maendeleo ya nchi hizo mbili ni fursa kwa kila upande.

Kuhusu uhusiano wa pande hizo mbili katika muongo uliopita, Waziri Mkuu huyo amesema uzoefu na nia halisi ni kudumisha kuheshimiana na ushirikiano wa kunufaishana, na kutafuta msimamo wa pamoja wakati wa kukabiliana na tofauti zilizopo.