Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja la Mataifa (WFP) limesema wafanyakazi wake 50 wamepoteza maisha wakati wanatoa misaada ya kibinadamu nchini Ethiopia mwaka huu. Kifo kilichotokea hivi karibuni kati ya vifo hivyo 50, ni dereva mmoja kutoka mshirika wa WFP kuuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Amhara.
WFP imesema hali ya ukosefu wa usalama imeathiri shughuli zake za kibinadamu katika sehemu mbalimbali nchini humo, na kuwa inaendelea kukabiliana na changamoto za ugavi kutokana na ukosefu wa usalama, vizuizi barabarani na uhaba wa mafuta, ambavyo vimeathiri ufanisi wa kazi wa shirika hilo.