Kenya yasema iko njiani kukabiliana na kuenea kwa jangwa
2024-06-18 08:59:04| CRI

Kenya imeadhimisha Siku ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani, wakati ikiendelea na kazi ya kukabiliana na misukusuko hiyo, na kufanikiwa kupanua eneo la misitu hadi zaidi ya asilimia kumi ya ardhi yake.  

Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu wa Kenya Soipan Tuya, aliyeongoza sherehe zilizofanyika Laikipia katika Bonde la Ufa nchini Kenya, amesema eneo la miti nchini Kenya imefikia asilimia 12.3 ya ardhi yake.

Waziri Tuya amesema hii ni hatua kubwa katika kukabiliana na kuenea kwa jangwa, kuvia kwa ardhi na ukame, amekuwa akizunguka nchi nzima kuendesha kampeni ya upandaji miti, na kwamba mkakati huo wa kihistoria imehimiza kurejesha mfumo ikolojia nchini Kenya.