Wataalamu wageni kusaidia kuchunguza ajali ya ndege ya Malawi
2024-06-18 09:27:51| CRI

Rais Lazarus Chakwera wa Malawi amesema serikali ya Malawi itaalika wataalamu wa kigeni kusaidia kuchunguza chanzo cha ajali ya ndege iliyosababisha kifo cha makamu wa rais wa nchi hiyo Bw. Saulos Chilima na maofisa wengine.

Akiongea kwenye mazishi ya kitaifa, Rais Chakwera amesema wataalam wenyeji wanaendelea na uchunguzi, na kusisitiza umuhimu wa uchunguzi wa kina ili kutoa majibu yanayaowasumbua watu wa Malawi na yeye mwenyewe.

Serikali imetoa wito wa kuomboleza kwa amani huku kukiwa na baadhi ya dalili za mvutano kufuatia nadharia za njama zinazoenea.