Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za kukomesha uharibifu wa dunia, wakati karibu asilimia 40 ya ardhi ya dunia inaharibiwa, na kila sekunde eneo la ardhi nzuri lenye ukubwa wa karibu viwanja vinne vya soka linaharibiwa.
Akiongea kwenye Siku ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani, Bw. Gutteres amesema usalama, ustawi na afya ya mabilioni ya watu hutegemea ardhi nzuri kusaidia maisha, njia za kujikimu na mifumo ya ikolojia, lakini binadamu tunaharibu dunia hiyo.
Amekumbusha kubwa ardhi yenye afya inatupatia karibu asilimia 95 ya chakula kinacholiwa duniani kote, pamoja na nguo na makazi, na pia inatoa kazi na riziki na kulinda jamii dhidi ya majanga ya ukame, mafuriko na moto wa msituni.