Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa jumuiya ya wahitimu wa Chuo cha Kijeshi cha Huangpu kuadhimisha miaka 100 ya chuo hicho na maadhimisho ya miaka 40 tangu jumuiya hiyo ianzishwe.
Kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati hiyo na mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Kijeshi, alitoa pongezi za dhati kwa jumuiya ya wahitimu wa chuo hicho na kuwasalimu wahitimu na jamaa zao walio nchini na nje ya nchi.
Kwenye barua yake Rais Xi amesema, Chuo cha Kijeshi cha Huangpu, kilichoanzishwa chini ya ushirikiano wa mara ya kwanza kati ya Chama cha Kuomingtang cha China (KMT) na Chama cha Kikomunisti cha China, ni cha kwanza kilichoandaa maofisa wa kijeshi kwa ajili ya mapinduzi ya China.
Rais Xi amehimiza jumuiya ya wahitimu wa chuo hicho kuenzi desturi ya kizalendo na kimapinduzi ya chuo hicho, kupinga kithabiti wafarakanishaji wanaotaka kuitenga Taiwan kutoka China, kuhimiza umoja wa kitaifa, na kuchangia busara na nguvu katika kutimiza ndoto ya China.