Mkenya ashinda Sh8.3 milioni kwa kuvumbua kifaa cha kutambua wadudu shambani
2024-06-18 14:09:48| cri

Mvumbuzi Esther Kimani, aliyeshinda Sh8.3 milioni kutokana na tuzo ya ubunifu wa Uhandisi barani Afrika iliyoandaliwa na Royal Academy of Engineering, ameahidi kuboresha kifaa kinachotumia kamera na miale ya jua kutambua wadudu na ugonjwa unaoangamiza vyakula shambani.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 32 aliunda kifaa hicho kwa kutumia teknolojia ya Akili Bandia. Bi Kimani ni mwanamke wa tatu barani Afrika na wa pili nchini Kenya kushinda tuzo hiyo ya kifahari baada ya Edmund Wessels pamoja na Anatoli Kirigwajjo kutoka Afrika Kusini kutajwa washindi pamoja wa 2023.

Bi Kimani alipokea Sh8.3 milioni (£50,000), kiasi kikubwa zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya Tuzo ya Afrika.