Kenya yasema bwawa lililojengwa na kampuni ya China litakuwa na manufaa mengi
2024-06-19 08:43:16| CRI

Waziri wa Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji kwa Kenya Bw. Zacharia Njeru amesema Bwawa la Thwake lililojengwa na kampuni ya China kwenye kaunti ya Makueni, linakaribia kukamilika, na kuanza kutumika kwake baadaye mwaka huu kutafungua njia ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi nchini Kenya.

Bw. Njeru amesema bwawa hilo linatarajiwa kuimarisha usambazaji wa maji, umwagiliaji, na uzalishaji wa umeme katika maeneo yenye ukame mashariki mwa Kenya.

Bwawa hilo limejengwa na kampuni ya Gezhouba ya China na kugharamiwa kwa pamoja na serikali ya Kenya na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), pia litasaidia kutatua suala la uhaba wa chakula na maji kwa kaya na mifugo.