Kampuni ya China yafungua kiwanda cha vifaa vya kupaua vilivyo rafiki kwa mazingira nchini Kenya
2024-06-19 08:42:36| CRI

Kampuni ya China inayotengeneza vifaa vya kupaua imefungua kiwanda kipya nchini Kenya ili kulipatia soko la Kenya vifaa hivyo vya bei nafuu, rafiki kwa mazingira na vya kudumu.

Akiongea mjini Machakos kwenye ufunguzi wa kiwanda hicho, meneja mkuu wa Kampuni ya SINOMA iliyofungua kiwanda hicho Bw. Wu Shuang, amesema Kenya na China zina uhusiano wa karibu wa kirafiki, na kampuni yake itatengeneza vifaa vya bei nafuu na vyenye ubora ambavyo vitakidhi mahitaji ya watu wa Kenya.

Gavana wa Kaunti ya Machakos, Wavinya Ndeti, amesema wanafurahi kuwa teknolojia inayotumika itabadilisha jinsi uwekaji wa mapaa unavyofanywa nchini Kenya, na kwamba kiwanda kitatoa fursa kwa vijana kujifunza jinsi teknolojia hii inavyofanya kazi.