Kampuni za China kushiriki katika maonyesho makubwa ya biashara ya Tanzania
2024-06-19 09:25:35| CRI

Kaimu mkurugenzi wa ukuzaji wa biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw. Tito Nombo amesema kundi la makampuni ya China litashiriki kwenye maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yatakayofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13.

Bw. Nombo amesema nchi nyingine 10 pia zinatarajiwa kushiriki katika maonesho hayo ya mwaka huu yenye kauli mbiu ya "Tanzania: Kituo Chako Bora Kwa Biashara na Uwekezaji."

Bw. Nombo amesema maonyesho hayo yanalenga kutangaza bidhaa na huduma, kuwasaidia waonyeshaji kufikia masoko mapya na kutafuta fursa mpya. Mfadhili mkuu wa maonyesho hayo ya biashara ni Kampuni ya mambo ya ugavi ya China iliyoko Afrika Mashariki, inayojihusisha na biashara ya kimataifa.