Wakenya milioni 1.9 katika maeneo kame wakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula
2024-06-19 09:29:17| CRI

Mamlaka ya Usimamizi wa Ukame ya Taifa ya Kenya NDMA imesema, watu wapatao milioni 1.9 nchini Kenya wanahitaji msaada wa chakula, wakati hali ikizidi kuwa mbaya kati mwezi wa Juni hadi Agosti.

Mamlaka hiyo imetoa ripoti mpya kwa mwezi wa Mei ikisema, watu hao wako katika kaunti 23 kame na nusu kame nchini Kenya, ambao wako katika hali ya kawaida ya ukame.

Mamlaka hiyo imesema hali inakadiriwa kuwa mbaya zaidi katika msimu wa June hadi Agosti kwenye baadhi ya kaunti kame isipokuwa sehemu chache.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, utapiamlo mkali umetokea katika kaunti mbalimbali, ambako watoto wapatao laki 8.5 wenye umri wa miezi 6 hadi 59 na wajawazito na mama wanaonyonyesha zaidi ya laki 1.2 wanakumbwa na utapiamlo na kuhitaji matibabu.