Rais Xi atoa maagizo muhimu kuhusu mapambano dhidi ya mafuriko na ukame
2024-06-19 08:46:01| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa maagizo muhimu kuhusu mapambano dhidi ya mafuriko na ukame.

Rais Xi amebainisha kuwa mvua kubwa zinaendelea kunyesha katika sehemu nyingi za kusini mwa China, na mafuriko na maafa ya asili yametokea katika mikoa ya Guangdong na Fujian na sehemu nyinginezo, na kusababisha vifo vya watu na hasara za mali. Kwenye baadhi ya sehemu kaskazini mwa China, ukame umetokea na kuenea kwa haraka.

Rais Xi ametaka juhudi zote zifanywe kukabiliana na majanga haya, kufanya kila kinachowezekana kutafuta na kuokoa watu wasiojulikana walipo au waliokwama, kuwahifadhi wahanga wa maafa, na kuhakikisha utaratibu wa uzalishaji na maisha na kupunguza hasara kadri iwezekanavyo.