Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini akutana na rais wa Russia
2024-06-19 09:27:46| CRI

Shirika la Habari la taifa la Korea Kaskazini limeripoti kuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo Bw. Kim Jong Un amempokea rais wa Russia Vladimir Putin aliyewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pyongyang kwa ziara ya kiserikali nchini humo.

Bw. Kim Jong Un ameeleza kufurahia kukutana tena na rais Putin baada ya siku 270 tangu wakutane katika kituo cha kurushia vyombo vya anga ya juu cha Vostochny mwezi Septemba mwaka jana. Rais Putin pia amemshukuru kiongozi huyu kumkaribisha katika uwanja wa ndege, na baada ya hapo, viongozi hao walifanya mazungumzo ya kirafiki katika Jumba la Wageni la Taifa la Kumsusan.

Shirika hilo pia limesema ziara ya rais Putin ina umuhimu mkubwa kuhimiza maendeleo ya kimkakati ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika siku zijazo.