Rais wa China afanya ukaguzi na utafiti mkoani Qinghai
2024-06-19 11:12:31| cri

Rais Xi Jinping wa China, jana amefanya ukaguzi na utafiti mkoani Qinghai, ambapo alitembelea Shule ya Sekondari ya Makabila ya Guoluo Xining na Hekalu ya Hongjue mjini Xining, ili kupata ufahamu kuhusu hali ya kukuza ushirikiano kati ya sehemu za mashariki na magharibi katika mambo ya elimu, kuimarisha wazo la elimu inayohudumia umoja wa kitaifa, na moyo wa uzalendo na uaminifu wa imani katika sekta ya dini ya Kibudha ya Tibet, pamoja na kukuza umoja na maendeleo ya makabila mbalimbali.