Afrika yahimizwa kukumbatia Akili Bandia kusukuma mbele maendeleo na kuwezesha nguvukazi ya Afrika
2024-06-19 09:28:34| CRI


 

Bara la Afrika limehimizwa kutumia fursa zinazoletwa na Akili Bandia (AI) kusukuma mbele ukuaji wa uchumi na kuwawezesha wafanyakazi wake wengi.

Wito huo umetolewa na Idara ya Maendeleo ya Umoja wa Afrika katika waraka wenye kichwa cha “Akili Bandia na Siku za Baadaye za Kazi Barani Afrika”. Ripoti hiyo imesema, Akili Bandia inatoa chombo chenye nguvu kwa kuunda siku za baadaye za kazi zenye heshima barani Afrika.

Ripoti hiyo pia imesema, kupitia kukabiliana na changamoto na kutumia fursa, Afrika inaweza kutumia AI kuhimiza ukuaji wa uchumi, kuwawezesha wafanyakazi wake vijana, na kuwa kiongozi katika maendeleo ya AI yenye wajibu wa kijamii. Idadi kubwa ya vijana barani Afrika na mfumo ikolojia wa teknolojia wenye uhai umetoa fursa kubwa kulifanya bara hilo kushiriki katika uvumbuzi wa teknolojia na maendeleo endelevu.