Rais wa Rwanda azishutumu nchi za Magharibi kutumia vigezo viwili vya demokrasia kabla ya uchaguzi
2024-06-19 08:47:07| CRI

Rais Paul Kagame wa Rwanda amezishutumu nchi za Magharibi kwa kutumia vigezo viwili vya demokrasia, kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mwezi ujao nchini humo.

Bw. Kagame, ambaye amekuwa Rais wa Rwanda tangu mwaka 2000 alisema hayo alipojibu swali kuhusu wakosoaji waliomshutumu kung’ang’ania madaraka.

Rais Kagame amesema demokrasia inahusu uhuru wa maamuzi, na kwamba hajui mahali popote ambapo demokrasia imefanikiwa wakati kanuni na maadili yake vyote vinaamriwa kutoka nje.

Kauli hiyo ya Kagame imetolewa siku kadhaa baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa idhini kwa yeye na wagombea wengine wawili kushiriki kwenye uchaguzi wa rais utakaofanyika mwezi ujao.