Mauzo ya bidhaa za Kenya kwa nchi za Afrika yaongezeka katika robo ya kwanza ya mwaka huu
2024-06-20 09:20:02| CRI

Benki kuu ya Kenya katika ripoti ya kiuchumi iliyotolewa jana imesema mauzo ya Kenya kwa nchi nyingine za Afrika yaliongezeka kwa asilimia 16.5 hadi shilingi bilioni 113.1 (kama dola za Kimarekani milioni 874) katika robo ya kwanza ya mwaka 2024 kutoka dola milioni 749 ya mwaka 2023 kipindi kama hicho.

Benki hiyo imesema mafanikio hayo yametokana na sera ya nchi hiyo kuruhusu watu kutoka nchi zote za Afrika iliyotangazwa na rais William Ruto wa Kenya mwezi Desemba mwaka 2023, na ilianza kutekelezwa mwezi Januari 2024, huku nchi hiyo likitarajia kupata mafanikio kutokana na Eneo la Biashara huria la Bara la Afrika.

Ripoti ya benki kuu imesema bidhaa nyingi kutoka Kenya ziliuzwa nchini Uganda, Tanzania na Rwanda, huku Misri, Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zikiwa na mahitaji makubwa.