Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing jana Jumatano kwenye mkutano wa wazi wa Baraza la Usalama kuhusu suala la Libya, amesema China inaunga mkono juhudi za kutatua masuala ya Afrika kwa njia za kiafrika, anaamini kwamba Libya inaweza kunufaika kutokana na uzoefu wa maafikiano ya Umoja wa Afrika, na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa uungaji mkono wa lazima kwenye suala hilo.
Balozi Dai Bing amesema mazungumzo ni njia pekee ya kutatua mvutano wa kisiasa wa Libya. China imefahamu kuwa pande mbalimbali za Libya zitakutana mjini Cairo kwenye duru ya pili ya mazungumzo ya kisiasa. Amesema anatarajia kuwa pande husika za Libya zitafuata mwelekeo sahihi wa utatuzi wa kisiasa, na kudumisha mazungumzo ili kuondoa tofauti zilizobaki na kuendelea kusukuma mbele mchakato wa kisiasa.