Russia na Korea Kaskazini zakubaliana kuungana mkono kama uvamizi utatokea
2024-06-20 14:03:08| cri

Vyombo vya habari vya Russia Jumatano vilimnukuu rais Vladimir Putin wa Russia akisema kuwa Russia na Korea Kaskazini zimekubaliana kuungana mkono kama ukitokea uvamizi kutoka nje.

Shirika la habari la Russia RIA Novosti lilimnukuu Putin aliposhiriki kwenye mkutano na wanahabari baada ya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un huko Pyongyang akisema kuwa, kwa mujibu wa makubaliano ya uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote yaliyosainiwa sasa hivi, Russia haitaondoa ushirikiano wake wa kijeshi na kiteknolojia na Korea Kaskazini.

Habari zinasema, Putin alisema makubaliano hayo ni hati ya mafanikio, ambayo inaweka malengo katika kuimarisha uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi mbili kwenye sekta mbalimbali. Ameongeza kuwa mchi zote mbili zinapinga kuweka vikwazo kwa malengo ya kisiasa, kwa kuwa vitendo hivyo vinadhoofisha mfumo wa kiuchumi na kisiasa duniani.